Laini ya Afya ya Akili ya Kitamaduni 1800 648 911

 

Kuunganisha lugha, tamaduni na huduma ya afya ya akili


Laini ya Afya ya Akili ya Kitamaduni inakuunganisha kwa wataalamu wenye uzoefu wanaoelewa utamaduni wako na wanaoweza kuwasiliana katika lugha yako.
Wakati unapopiga simu kwenye 1800 648 911, utaongea na mtaalamu wa afya anayeweza:

  • kutoa ushauri juu ya jinsi ya kuboresha ustawi wako na afya yako ya kiakili
  • kukusaidia kupata huduma za afya ya kiakili katika jumuiya yako
  • kukusaidia wewe kumtunza mtu mwingine mwenye shida ya afya ya kiakili

Unaweza kupiga simu kwenye 1800 648 911 kwa Jumatatu hadi Ijumaa saa 3:00 asubuhi (9am) hadi 10:30 jioni (4.30pm)


Laini ya Afya ya Akili ya Kitamaduni ni huduma ya msaada wa afya ya kiakili.

Ikiwa mtu anahitaji usaidizi wa mara moja, pigia simu Sifuri Mara Tatu (000).

Kwa usaidizi na ushauri wa afya ya akili na katika jioni na wikendi, piga simu kwenye Laini ya Afya ya Akili (Mental Health Line) kwenye 1800 011 511.

Simu hii inapatikana masaa 24 kwa siku, siku saba kwa wiki. Ikiwa unahitaji usaidizi wa lugha kuongea na huduma hii, pigia simu Huduma ya Utafsiri na Ukalimani (Translating and Interpreting Service - TIS National) (TIS Taifa) kwenye 131 450 na omba kwa Laini ya Afya ya Akili. Maelezo juu ya ustawi na afya ya kiakili katika lugha yako yanapatikana kwenye tovuti ya Kituo cha Afya ya Akili ya Kitamaduni: www.dhi.health.nsw.gov.au/tmhc

 


Postcard

Transcultural Mental Health Line Postcard  Swahili
Download the Transcultural Mental Health Line Postcard in Swahili here (PDF 839.7KB). 

To order hard copies of the Transcultural Mental Health Line Postcard in Swahili email us at [email protected]

 


View and download all Transcultural Mental Health resources in Swahili here